Katika kijiji kimoja duni, binti mmoja aliyeitwa Lydia alikuwa akitengeneza bustani ya maua yenye kupendeza kando ya nyumba yao ya msonge iliyojengwa kwa matope na kuepuliwa kwa majani makavu. Licha ya umaskini wao, nyumba hiyo ilikuwa ya kipekee; Lydia alikuwa amechora maua mazuri kuta zake, na kuifanya ivutie kiasi kwamba wapita njia walisimama kupiga picha.
Mama yake Lydia alifariki miaka mingi iliyopita, akimwacha baba yake akimlea peke yake. Baada ya miaka kadhaa ya upweke na majukumu mazito ya kulea, baba yake aliamua kuoa mke mwingine Lydia akiwa na umri wa miaka saba tu. Mwanzoni, mama huyo wa kambo alionekana kuwa mzuri sana, akimlea Lydia kwa upendo na kufuta kabisa dhana ya ukatili wa mama wa kambo.
Hata hivyo, mambo yalianza kubadilika baada ya yule mama kujifungua binti yake mwenyewe, Lorrah. Lorrah alipokua, hakuwa na mvuto wala urembo wa asili kama Lydia, jambo lililochochea wivu mkubwa moyoni mwa mama yake. Lydia alikuwa na umbo zuri na rangi ya kuvutia tingu utotoni, kiasi kwamba hata bila kupaka mafuta alipendeza sana.
Mbele ya baba yake, mama huyo alijifanya kumpenda sana Lydia. Lakini baba yake akiondoka tu, alimnyanyasa na kumtesa vikali, akimtishia kuwa akimwambia baba yake, angemwua yeye pamoja na baba huyo. Kwa uoga wa kitoto, Lydia aliamua kukaa kimya na kupambana na mateso hayo peke yake.
Ili kukwepa kero za mama yake, Lydia alikuwa mchapakazi sana, akitumia muda wake wa ziada kutengeneza bustani, kuchora na kuimba. Aliona muziki kama faraja ya moyo wake, huku michoro na maua vikimpa tabasamu la mara kwa mara lililomsaidia kusahau machungu ya kuteswa na mama yake wa kambo.
Soma, sikiliza na tazama sehemu zote za hadithi, katuni na video kwenye tovuti ya Story Space.
Endelea Kwenye Tovuti© 2026 Story Space