Nilikuwa nimemaliza shahada yangu ya kwanza ya uuguzi na ukunga katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Sikuwa daktari, bali nesi aliyepikwa vizuri na kujiandaa kutoa huduma kwa jamii. Baba yangu alikuwa mwanajeshi mwenye cheo cha Kapteni nchini Tanzania. Mara tu niliporudi nyumbani, alitaka nijishikize kwenye hospitali ya jeshi iliyopo ndani ya Kambi ya Oljoro mkoani Arusha, nikiwa nasubiri ajira rasmi ambazo alikuwa akinifanyia mchakato.
Nilikuwa binti mrembo sana, na nilijua hilo bila shaka. Sikuwa mweupe, bali nilijaaliwa ngozi nyeusi ya kuteleza, isiyo na chunusi wala doa tangu kuzaliwa kwangu. Licha ya uwezo wa kifedha wa baba yangu, mafuta yangu ya kila siku yalikuwa ya mgando ya Vaseline tu. Nilikuwa na umbo maridadi la wastani, nyonga zilizochongwa vizuri, na miguu ya kuvutia ambayo kila mtu aliisifia. Hata hivyo, mimi ni binti wa Kiislamu; mavazi yangu ya kila siku yalikuwa abaya za heshima, na kazini nilivaa suruali pana na shati refu lililopita magoti. Nilishikilia msimamo wangu wa kutoguswa na mwanamume yeyote hadi atakapokuwa halali yangu.
Uwepo wangu kambini ukawa kivutio kikubwa kwa kila mwanamume. Siku moja nikiwa kwenye majukumu yangu, nilimsikia mmoja wa wanajeshi akitania wenzake, "Huyu sasa ni demu wangu. Muulizeni, na akikataa nitafanya kazi zenu wote kwa wiki nzima!" Nikichukulia jambo hilo kama utani wa kawaida wa kambini, walipokuja kuniuliza, nilijibu kwa tabasamu, "Ndiyo, ni mwanaume wangu na nampenda sana."
"Umeshawishika na nini kwa huyu mpuuzi?" mmoja wao aliuliza kwa mshangao. Nilijibu kwa kujiamini, "Yeye ni muungwana sana, na mwanamke yeyote aliyekamilika hawezi kukataa kuwa na mwanamume kama yeye." Yule mwanajeshi niliyemtetea alitabasamu kwa furaha na kusema, "Wow, binti una maneno matamu sana!" Kiukweli, sikuwa namjua hata jina lake, na nilikuwa na uhakika yeye pia hanijui, lakini tangu wakati huo, wenzake waliamini kabisa kuwa tuna uhusiano.
Soma, sikiliza na tazama sehemu zote za hadithi, katuni na video kwenye tovuti ya Story Space.
Endelea Kwenye Tovuti© 2026 Story Space